Wednesday, November 2, 2016

Rapper Mabeste amefunga ndoa

Msanii wa Bongofleva William Ngowi ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la Mabeste ameamua kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu na mzazi mwenzake Liser Fickensher, Mabeste amefunga ndoa mpenzi wake huyo ambaye pia ni mama wa mtoto wake Kendrick.
sv1
Kupitia katika instagrama account yake ya @mabeste_tanzania na instagram account ya mkewe @lisa_fickenscher wawili hao leo October 31 wameshea picha za harusi yao pamoja na picha wakiwa kanisani wakati wa kufunga ndoa.
sv3

FA wamemshtaki kocha Jose Mourinho kwa utovu wa nidhamu

Chama cha mpira wa miguu cha England FA kimemshtaki kocha Jose Mourinho kwa utovu wa nidhamu alioonesha katika mechi ya Man United dhidi ya Burnley jumamosi ya, Oktoba 29,2016.
39d8778800000578-0-image-a-2_1477907602312
Imeripotiwa kuwa kipindi cha mapumziko Kocha huyo alitumia maneno mabaya kwa mwamuzi Mark Clattenburg,na kipindi cha pili akapelekwa jukwaani kwa mashabiki kutokana na kosa hilo.
Jose alikuwa mkali kwa mwamuzi huyo akidai kwa nini timu yake haikupewa penati pale Matteo Darmian alipochezewa vibaya na Jon Flanagan katika eneo la hatari.
FA imemtaka Jose kujibu shtaka hilo kabla ya siku ya ijumaa ya juma hili

Rais Magufuli ampongeza Rais Kenyatta kwa ujenzi wa barabara ya kisasa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta wamezindua barabara ya Southern Bypass huku Rais Magufuli akisema wananchi wanahitaji maendeleo na hayo ndio yenyewe.
14915571_1440392175989331_5633888333426358079_n
Akizungumza katika sherehe hiyo, Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambapo amesema haitawasaidia wananchi wa Kenya tu, bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia Nairobi.
“Wananchi wanahitaji maendeleo na haya ndio maendeleo, barabara hii itasaidia kuinua uchumi na itasaidia masuala ya kijamii,” alisema Rais Magufuli.
Barabara hiyo ina urefu wa kilometa 28 na inaunganisha maeneo mbalimbali ya jiji la Nairobi. Uzinduzu huo umefanyika katika eneo la Karen nje kidogo ya jiji la Nairobi.
Hizi ni baadhi ya picha katika ufunguzi wa barabara hiyo:
3
5
6

Tuesday, November 1, 2016

WhatsApp yaanzisha video call kwenye simu za Android


Baadhi ya watumiaji sasa wanaweza kupiga simu za video kutumia WhatsApp version ya Android.
annoying-phone-calls
Kwa sasa version hiyo inapatikana kwa watumiaji wachache wa simu za Android, huku wale wenye simu za iPhone wakiwekwa pembeni. Huduma bado ipo kwenye majaribio (beta version).
Uwezo huo wa WhatsApp kupiga simu za video unaifanya app hiyo ishindane na Facetime ya Apple.

Monday, July 15, 2013

BINTI KIZIWI ATUPWA JELA MIAKA MITANO BAADA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA


MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa biashara hiyo haramu.

Hivi karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’ amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda kortini mara moja Ijumaa iliyopita.
 

Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’, Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata la ‘unga’.

Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita. 


Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.


Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo,mwandishi  wetu  alilazimika  kuwatafuta  ndugu  zake  ili  kuujua  ukweli


Kwa  mujibu  wa  maelezo  ya  ndugu  yake, Binti  kiziwi  hajanyongwa  bali  ametupwa  jela  miaka  mitano.


“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”


DEMU WA KANUMBA NAYE ASOTA RUMANDE
Msichana anayejulikana kwa jina la Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu wa Kanumba’ yeye bado anasota kwenye Gereza la Segerea, Dar kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170.


Saada alidakwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Juni 24, mwaka huu. 


Kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza, Juni 29, mwaka huu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.



 MSANII BONGO MUVI ‘ASUBIRI KITANZI’ MISRI
Wakati mlolongo wote ukiwa hivyo, mrembo aliyewahi kushiriki filamu Bongo, Sharifa Mahamoud (27) naye anashikiliwa katika gereza moja nchini Misri wakati kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ikirindima nchini humo

WANAJESHI 7 WA TANZANIA WAMEUAWA HUKO DARFUL- SUDAN


Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa. 
 
Taarifa zilizotufikia jana  zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.
Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.
Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo.
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.
Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji.
Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.

Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur. 
Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur.
Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC.

Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanzania imepeleka wanajeshi 850.

“Tanzania imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na ushauri kwa nchi nyingi,” alinukuliwa Kanali Mgawe, na kueleza kuwa majeshi ya Tanzania yamekuweko katika vikosi vya kulinda amani huko Lebanon, Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya Comoro na Liberia. Liberia waliuawa wanajeshi wa Tanzania 11.
 “Tanzania daima haiendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa,” alisema